
Tetesi za soka Ulaya
Timu ya Bayern Munich itakabiliana na ushindani kutoka kwa klabu mbili za Ligi Kuu ya Uingereza wakati wa kumnunua kiungo wa Fulham na Ureno, Joao Palhinha (28), mwezi Januari - limeandika gazeti la Telegraph.
Bayern wanaweza kumkosa kiungo wa kati wa Bayefdcer Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani, Florian Wirtz pia, kwani Manchester City na Liverpool zina nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, mtandao wa 90min unaeleza.
Mshambuliaji wa Gremio na Uruguay, Luis Suarez (36), anatazamiwa kuungana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona, Lionel Messi katika klabu ya Inter Miami kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kocha wa zamani wa Wolves, Julen Lopetegui alikataa kandarasi ya pauni milioni 15.4 za Uingereza kwa msimu kutoka kwa timu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia akitaka kusalia kwenye Ligi ya Kuu ya Uingereza, huku Manchester United ikiwa miongoni mwa vilabu vinavyohusishwa kutaka kumwajiri Mhispania huyo.
Kitahitajika kitita cha pauni milioni 60 kwa Aston Villa kufikiria kumuuza Douglas Luiz ifikapo mwezi Januari, huku Arsenal ikionyesha nia ya kutaka kumnunua kiungo huyo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 25.
Arsenal na Liverpool zote zilituma mawakala kumtazama beki wa pembeni wa Bayer Leverkusen na Uholanzi, Jeremie Frimpong (22).
Real Sociedad wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza, Mason Greenwood (22), ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Getafe.